Jugo Media
JUGO MEDIA NETWORK ni chombo cha uinjishaji kupitia mtandao kilichoanzishwa miaka minne (4) iliyopita (19/02/2019) katika chumba kidogo cha kontena la Kwaya ya Familia Takatifu Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Malengo makubwa ya Jugo Media Network ni kuwalisha kiroho waamini wa Kanisa Katoliki na wakirstu wote kwa vipindi mbalimbali vya kiroho, Misa Takatifu na homilia za maaskofu na mapadre kwa kutumia mitandao ya kijamii ambayo kwa dunia ya sasa imeonekana kuwa na upotovu mkubwa wa maadili hasa kwa vijana lakini pia ndio tasnia inayokuwa kwa kasi Zaidi ulimwenguni, hivyo mwanzilishi, Ndugu Ibrahim Gores akajikita Zaidi na kundi kubwa la vijana na watu wa rika zote walioko mitandaoni kuwawezesha kuweza kupata neno la Mungu katika Mazingira yao walipo, muda wowote ule. Channel Hii inaongozwa na kauli Mbiu Jugo Media - Injili Kiganjani Mwako
152000 subscribers

Videos