Prophet Hebron Wilson Kisamo
MTUME NA NABII HEBRON WILSON KISAMO ni Mtumishi wa MUNGU wa kweli ambaye YESU amemchagua amtumikie yeye ili kuukomboa ulimwengu huu ambao umepotea na shetani ameumiliki kwa asilimia 98%, Kwani wale Waliokuwa watumishi wa YESU wamemsaliti 98% na Wameamua kuwa wachawi na waganga kwa kwenda kuzimu, na kumtumikia shetani, watumishi wengi kwa sasa wamefanya kanisa ni mahali pa biashara, kunyanganya watu vitu vyao na pesa zao makanisani na kumfanya YESU aonekane ni mnyan’ganyi na mwizi huku wakiwaombea watu kwa kuwadai pesa, wakati YESU yeye amesema katika Neno lake katika kitabu cha Mathayo 10:8 “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.” lakini wao wanawadai watu pesa eti ndio wawafanyie maombi, kwa midomo yao humtaja kama wanampenda YESU ila mioyoni mwao hawapo na yeye, wamekuwa watumishi wa pesa, wamekuwa wakitenda miujiza lakini siyo ya YESU ni miujiza ya shetani, na hao ni kati ya wale ambao siku ya mwisho YESU atawakataa.
56500 subscribers

Videos