FDT Module 4 Utunzaji wa Shamba la Miti- Kiswahili



1
3507

Baada ya kupanda miti kwenye shamba utunzaji wa miti ni muhimu ili kuimarisha ustawi wa miti hiyo. Miti ya milingoti/mikaratusi inahitaji usafi zaidi kuliko mipaina. Njia nyingine ni kupalilia visahani au kufyeka majani yote shambani. Kupogolea (Pruning) ni muhimu sana kwa miti ya mipaina kwani miti ya milingoti haihitaji kupogolewa kwa sababu huwa inajipogolesha yenyewe (self-pruning). Kupunguzia miti (thinning) ni moja ya hatua muhimu kwenye utunzanji wa shamba la miti. Njia za kuzuia moto (Fire Lines) zinatakiwa zitengeneze kila mwaka baada tu ya msimu wa mvua kuisha. Pia ulinzi wa magonjwa mbalimbali lazima uwepo ili kuhakikisha miti yenye tatizo inatibiwa au kukatwa na kuchomwa ili kudhibiti kuenea kwa magonjwa shambani. Ila kwa sasa tunabahati ya kutokuwa na magonjwa mengi nchini mwetu hivyo hili sio la kuhofiwa sana. Kwa maelezo zaidi tembelea: http://smartforestry.blogspot.com/

Published by: pelezi ruffo Published at: 7 years ago Category: مردم و وبلاگ