DC MSHAMA NA VIONGOZI WA TFS WAVAMIA MSITU WA DUTUMI KIBAHA PWANI TANZANIA



0
157

DC MSHAMA NA VIONGOZI WA TFS WAVAMIA MSITU WA DUTUMI KIBAHA PWANI TANZANIA Na Omary Mngindo, Dutumi, Kibaha Pwani Tanzania- Des 7 MKUU wa wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani, Tanzania Assumpter Mshama akiambatana na Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Mashariki Carolin Malundo wamefanya ziara ya kushtukiza katika Hifadhi ya Msitu uliopo Kijiji cha Dutumi Kata ya Dutumi wilayani humo. Pia msafara huo umehusisha Meneja Msaidizi Lasirimali za Misitu Benadetha Kadala, Meneja wilaya ya Kibaha Peter Nyahende, Mkuu wa Polisi Wilaya Mlandizi Kasta Ngonyani, Maofisa wa jeshi hilo pamoja na viongozi mbalimbali wa TFS ambao walitembelea msitu huo uliopo kijijini humo na kukuta watu wakiwa wameweka makazi ndani ya eneo hilo linalodaiwa ni Hifadhi ya Msitu. Akiwa katika ziara hiyo ya kushtukiza kwenye msitu huo, Mkuu huyo ameshangazwa alipoona agizo lake la siku 30 alizowapatia wananchi hao kuondoka likiwa halijatekelezwa huku wananchi hao wakiendelea kukata miti na kuchoma mkaa. Akizungumza na wananchi hao, Mshama aliwataka wafungashe mizigo yao wapakie kwenye lori linalomilikiwa na TFS aina ya Isuzu lenye namba za usajili STK 2409 lakini nao wakatoa utetezi wao wakieleza kwamba baada ya kuondolewa walikokuwa awali, walipeleka barua wakiiomba Serikali ya kijiji iwapatie eneo la muda hapo walipo hivi sasa. MWISHO.

Published by: BILL MEDIA Published at: 6 years ago Category: مردم و وبلاگ