UKIONA MANYOYA UJUE KALIWA, YANGA 5, SIMBA 2



0
125

UKIONA MANYOYA UJUE KALIWA, YANGA 5, SIMBA 2 Na Omary Mngindo, Kibaha, Pwani- Agosti 14 TIMU ya soka ya Yanga Veteran ya Kibaha kwa Mfipa Mkoa wa Pwanu Jumapili ya Agosti 12 imeifunga Simba Veterani kwa mabao 5-2 katika mchezo maalumu ulioandaliwa na Mwamuzi Mstaafu Mbwana Mikoi. Katika mchezo huo uliolenga kuwapatia burudani wakazi wa eneo hilo na vitongoji vyake, ulipigwa katika uwanja wa kwa Mfipa mjini hapa, ukichezeshwa na Mwamuzi Yassin Ally kisaidiwa na Idrissa Juma na Hamisa Mussa. Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao kunako dakika ya 37 mfungaji akiwa Abdallah Mkopoka baada ya mabeki wa Yanga Veteran kushindwa kumdhibiti mfungaji aliyeupiga mpira ukamshinda mbinu kipa Juma Magoma. Timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji kadhaa ambayo hata hivyo Yanga ndio iliyonufaika ambapo ilijipatia bao la kusawazisha kunako dakika ya 88 mfungaji akiwa Abdul Rajabu aliyeingia dkika 5 kabla ya kupachika mpira huo wavuni. Baada ya kipyenga cha mwamuzi Yassin kuhitimisha dakika 90, hatua ya mikwaju ya penati ndipo ilipoingia ambapo hata hivyo nusura ivunjike baada ya Simba kumbadilisha mchezaji wa ndani kuwa kipa wakidai Abass Hussein aliyelinda lango wakisema ana uoni hafifu. Katika hatua hiyo ndipo Yanga Veteran iliibuka na ushindi huo kwa kupata penati 4 huku Simba wakipata moja, walioifungia Yanga ni Abdul Rajab, Abdallah Zungu, Athumani Abdallah na Michael Mhando. Penati ya Simba Veteran mfungaji Kondo Said, baada ya mchezo huo mgeni rasmi Goodluck Manyama Mwenyekiti Serikali ya Mtaa wa Mwendapole B alikabidhi zawadi za sabuni miche 15 kwa Zungu nahodha wa Yanga wakati Rajabu Chepe wa Simba alikabidhiwa sabuni za kuogea 15. MWISHO

Published by: BILL MEDIA Published at: 5 years ago Category: مردم و وبلاگ