KRISTO PASKA YETU AMECHINJWA SADAKA (SEKWENSIA YA PASAKA) - NYIMBO ZA PASAKA

73.4 K


14

Kristu Paska yetu, amechinjwa sadaka; tuile karamuye, na twimbe Aleluya Aliyejitoa, sadaka ya Paska, wakristu wamtolee, sadaka ya Sifa. Mwanakondoo aliwakomboa kondoo, Kristu asiye na dhambi amewapatanisha na Baba, watu wenye dhambi. Mauti na uzima, vimeshindana ajabu; Mkuu wa uzima aliyekufa, atawala mzima. Utuambie Maria, uliona nini njiani? Niliona kaburi la Kristu Mzima, na Utukufu wa aliyefufuka. Mashahidi ni Malaika, Leso ya uso na mavazi Kristu tumaini langu kafufuka, awatangulia Galilaya. Twajua Kristu amefufuka, kweli katika wafu Ewe Mfalme mshindaji, Utuhurumie. Amina Aleluya, Amina Aleluya *2

Published by: Jugo Media
Published at: 3 years ago
Category: موسیقی